EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mpoto kufanya kolabo na Banana Zorro ‘Sizonje’

Mrisho Mpoto (kulia) akiwa na Banana (kushoto) wakisikiliza kazi yao

 

Msanii wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, jumatano hii anajipanga kuachia wimbo mpya uitwao ‘Sizonje’ akiwa amemshirikisha Banana Zorro.

Mpoto ameiambia tovuti ya Bongo 5 jumatatu hii, kazi hiyo iliyotayarishwa katika studio yake chini ya producer Allan Mapigo, ni kazi bora itakayokonga roho za mashabiki wake.

“Nimefanya kazi ambayo kila mtu akiisikiliza atatoka na kitu chake kwasababu ni kazi ambayo nimetumia muda mwingi kuiandaa”, alisema. “Sizonje ambaye nazungumzia kwenye hii nyimbo ni mtu, yaani hata wewe kwenye kazi yako, nyumbani, hospitali unaweza ukawa Sizonje. Kwahiyo ni wimbo ambao kila mtu akisikiliza atatoka na kitu”.

Aliongeza “Hii kazi ni ya yule Mrisho Mpoto wa Nikipata Nauli kazi ambayo mpaka leo mtu akiisikiliza anatamani zaidi kuendelea kuisikiliza ili aelewe nini kinachoendelea kwenye hii dunia”.

Mrisho mpoto pia aliwahi kumshirikisha Banana katika wimbo wake wa Nikipata Nauli.

Leave your comment