EXCLUSIVE (TANZANIA) –Kila ninachomiliki ni halali na nimepata kwa pesa yangu - Masanja
15 January 2016

Mchekeshaji wa Orijino Komedi na mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji amesema kila anachomiliki amaekinunua kwa pesa yake halali huku akishangaa kwanini watu wameshtuka kumuona akimiliki BMW yenye plate namba ya jina lake.
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds Tv Ijumaa hii, Masanja amesema anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli.
“Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha usafiri cha kunitoa pointi moja kwenda nyingine”, alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli”, alijinadi Masanja.
Na kuongeza “Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia”.
Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari la thamani si kitu cha ajabu, kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara yake moja tu.




Leave your comment