EXCLUSIVE (TANZANIA) – Q Chief kumaliza tofauti kati yake na meneja wake Mhonda
15 January 2016

Baada ya msanii wa Bongo Fleva Q Chief kutangaza kujiondoa katika kampuni ya QS J Mhonda, hatimaye mwanamuziki huyo na kampuni hiyo wamemaliza tofauti zao baada ya kukutana na kufanya mazungumzo.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo bwana Mhonda amesema kuwa wakati Q Chief anatangaza uamuzi wa kujiondoa kwenye kampuni yake hakuwepo jijini Dar, hivyo aliporejea Chillah aliomba kuonana nae ili kutafuta suluhisho.
“Ofcoz tulikutana nakumbuka na mimi nilikuwa naendelea na shughuli zangu, nikapata ujumbe kuwa aliomba tuonane nae..nimekutana nae”, alisema Mhonda kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.
Baada ya Mhonda kukutana na Chillah amesema aligundua kulikuwa na misunderstandings tu kwa pande zote mbili ambazo waliweza kuziweka sawa.
“Nilichogundua baadae ni kwamba kulikuwa na misunderstandings, unajua wakati vitu vimetokea mimi nilikuwa siko Dar es salaam nilikuwa niko mikoani .. kwahiyo kuna vitu ambavyo yeye alihisi viko hivyo kumbe ndivo sivyo. Sasa wakati tulipokutana alikuja politely si vile ambavyo nilikuwa nimetarajia kama ambavyo alikuwa ameongea kwenye radio”, alisema Mhonda.
“Nikajaribu kumweleza kile ambacho mimi nakifahamu, kwahiyo ikaonekana kwamba kumbe yeye alielewa tofauti, na mimi pia nilivyosikia redioni sikuweza kumwelewa kwa haraka kwanini ameweza ameweza kutokea kwenye media na kuongea vitu vya namna hiyo”, aliongeza Mhonda.
Baada ya mazungumzo yao Mhonda amesema muafaka uliweza kupatikana na kumsamehe Q Chief kwa yaliyotokea.
“Kwahiyo mwisho wasiku tumeyamaliza mimi kwangu sina kinyongo nimemsamehe, unajua katika hali ya kawaida huwezi kuendelea kukaa na kitu au unaweza usije ukaacha kumsamehe mtu wakati hata kwenye vitabu vya dini tunafundishwa kusameheana”.




Leave your comment