EXCLUSIVE (TANZANIA) - Nikipata mpenzi mpya nitatangaza mwenyewe - Shilole

 

Mwanamuziki Shilole a.k.a Shishi baby amesema baada ya kuachana na Nuh Mziwanda bado nafasi ya moyo wake haijapata mtu mwingine wa kuziba nafasi yake.

Zimekuwepo tetesi kuwa Shishi baby anatoka na msanii mwingine wa Bongo Fleva, Nyauloso zamani alikuwa kifahamika kama Bonge la nyau, huku wengine wakisema ana mahusiano na msanii wa Uganda Eddy Kenzo.

"Mimi sijapata mpenzi mpya mimi nipo tu, mpenzi mpya nitasema mwenyewe kwa mdomo wangu mimi" Shishi ameeleza kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM. "Nifanye interview niseme jamani nina mpenzi mpya, lakini saivi msisikie rumors zinazotokea subirini mimi niwahakikishie" alisema shilole.

Kuhusu Eddy Kenzo, Shilole amesema ni kama kaka yake lakini wanawasiliana sana na kuongeza endapo urafiki wao utazaa penzi basi atatangaza rasmi. 

Tazama hapa baadhi ya picha za mpenzi wa zamani wa shilole, Nuhu Mziwanda;

Shilole akiwa na Nuh

Nuh

Leave your comment