EXCLUSIVE (TANZANIA) – Shilole aongelea tetesi za yeye na Eddy Kenzo(Uganda) kuwa na uhusiano
11 January 2016

Msanii Eddy Kenzo wa Uganda alimuandikia wimbo maalumu Shilole na kuupa jina la mrembo huyo ‘Shilole’. Muimbaji huyo amesema Kenzo ni mtu anayempenda tangu zamani japo hiyo haimaanishi kuwa ni wapenzi.
“Eddy Kenzo nadhani nilikuwa Nigeria akanicheki, ilikuwa zamani sana ni kaka tu ambaye alikuwa na mapenzi na mimi. Mpaka mtu alifika stage kuandika wimbo kwaajili yangu ni mtu ambaye ana mapenzi”, amesema Shilole.
“Ni wimbo wenye feeling, mzuri lakini sio kusema kwamba ndio mpenzi wangu kama mnataka iwe hivyo tutaangalia” aliongeza.
Hivi karibuni mrembo huyo aliachana na mpenzi wake wa miaka mitatu, Nuh Mziwanda kutokana na sababu ambazo hajaziweka wazi.
Source: Bongo5




Leave your comment