EXCLUSIVE (TANZANIA) – The Industry kuongeza gharama za kurekodi baada ya kuboreesha studio – Nahreel
8 January 2016

Msanii na matayarishaji wa muziki wa ‘The Industry’ Nahreel amepandisha gharama za kurekodi muziki kwenye studio yake kutokana na ukarabati mkubwa alioufanya.
Nahreel ambaye mwaka 2015 ametengeneza hits mbalimbali kama ‘Game’ ya Navy Kenzo, ‘Nana’ ya Diamond, ‘Don’t Bother’ ya Joh Makini na nyingine nyingi. Msanii huyo ameiambia Clouds FM kuwa kutokana na ukarabati alioufanya katika studio yake, ameona aongeze bei ili kuendana na gharama alizotumia kuboresha.
“Ukarabati huo unaoendelea unafanyika kwa kiwango kikubwa sana, kuanzia mazingira hadi vifaa vya studio vimekuwa vya kisasa. Lengo ni kutengeneza ngoma kali na zenye ubora zaidi na kuhusu price za kurekodi track zimebadilika kidogo ila nisingependa kuweka wazi upande huo coz unaweza kuletewa kazi kubwa na msanii au mtu yoyote ikawa hailingani na bei niliyoitaja” , amesema Nahreel.




Leave your comment