EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mabadiliko katika muziki kwa sasa ni lazima – MwanaFA.

Rapper MwanaFA amewataka mashabiki wa muziki nchini kuacha tabia ya kuwalazimisha wasanii kufanya kila kitu wanachokitaka hata kama kikiwa hakina mantiki kwa wakati huo.

Msanii huyo aliyeachia video yake mpya ya ‘Asanteni Kwa Kuja’, amekiambia kipindi cha 360 cha Clouds TV kuwa msanii ndiye anyetakiwa kumbadilisha shabiki kwa kumpa vitu tofauti tofauti.

“Mashabiki wanataka kuendesha muziki kitu ambacho sio sawa na sioa sahihi” alisema Mwana FA.

“Ukienda kule kwenye page za Instagram ambako mashabiki wanaweza kukufikia kiurahisi unaweza ukapata lawama kwanini haubadiliki una sound kama old school rapa au mwingine anataka ubaki kama ulivyokuwa unarap zamani bila kujua sasa hivi tupo mbele zaidi”.

“Muziki sio kama ni jiwe, tuuchukulie kama mti unakuwa na changes zinatokea. Lazima tubadilike ukiangalia video zangu sidhani kama unataka tena nifanye kama ile ya ‘Mabinti’.  So ni lazima watu wakue, dunia inaenda kasi na muziki unakuwa ni lazima ubadilike. Kwahiyo mtu akiniambia hataki nibadilike anataka nibaki nilivyokuwa, sielewi” alisisitiza FA.

Leave your comment