EXCLUSIVE (TANZANIA) – Q Chief avunja mkataba na kampuni ya QS J Mhonda! Jua ni kwanini?
7 January 2016

Staa wa muziki nchini, Abubakari Katwila maarufu kama 'Q Chief' amevunja makataba wake na label ya muziki ya QS J Mhonda kwa madai kuwa kuna baadhi ya vitu haviendi sawa.
Q Chief amesema ameamua kujiondoa rasmi kwenye label hiyo ili asimame mwenyewe.
“Mimi bwana naomba uwaambie mashabiki wangu pamoja na watanzania, sipo tena na QS J Mhonda” amesema Q Chief. “Nimeamua kujitoa kwasababu kuna vitu haviendi sawa, sasa siwezi kuendelea kukaa bora nijitoe”.
Ambapo kwa upande wa mkurugenzi wa kampuni hiyo QS J Mhonda ameeleza kilichotokea na kusema, “Kilichomuuziza Q Chief ni kuona nawasaidia wasanii wengine”.
“Mimi kuwasaidia wasanii au watu mbalimbali ni sehemu ya masha yangu sasa yeye amekuwa akisema hadharani mbele ya wasanii wangu wadogo kwamba hawapendi kwamba hapendi hata kuwaona wasanii wachanga anatamani hata kuwapiga bastola ili asiwaone kabisa. Nimejitaidi sana kumweka sawa ili aendane na mimi au kampuni yangu lakini haonekani kubadilika na anaonesha roho mbaya kwa wenzake tena ya wazi” ameongeza.
“Hivi karibuni niliamua kumuongeza Mzee Yusuf katika kampuni yangu yaani kuwa miongoni kati ya wasanii wangu na nikampeleka Afrika Kusini kwaajili ya video yake mpya. Q Chief akakasirika kuona nafanya hivyo wakati hata kwake nafanya hivyo hivyo na kuzidi. Kwahiyo sasa mimi binafsi hiyo taarifa imenistua kwasababu tayari nimeshatumia zaidi ya milioni 60 mpaka sasa na bado anakaa kwenye nyumba yangu. Nikimpigia simu ananiambia ‘ongea na mwanasheria wangu’. Sasa mimi binafsi siwezi kuongelea hili suala na ni hatua gani tutazichukua lakini naomba ongea na mwanasheria wetu atakuwa na kauli”.
Ambapo mwanasheria wa kampuni hiyo Joseph Mhina, alidai mkataba ndio utakaomhukumu msanii huyo kwani kila kipengele kinaeleza hatua za kuchukua endapo mteja atakiuka utaratibu.
Akiwa na kampuni ya QS J Mhonda, Q Chief amefanya video kubwa mbili nchini Afrika Kusini na director Adam Juma.
Source: Bongo5




Leave your comment