EXCLUSIVE (TANZANIA) – Studio ya Professor Jay Kuhamia Mikumi

 

Msanii mkongwe wa Hiphop Joseph Haule maarufu kama Professor Jay na mbunge wa Mikumi amesema ana mpango wa kuhamisha studio yake ya Mwanalizombe kwenye jimbo lake ili aweze kutekeleza ahadi ya kuinua Sanaa.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania Jumatatu hii, Professor Jay alisema moja ya ahadi alizowaahidi wakazi wa Mikumi kwenye kampeni zake ni kuibua vipaji vipya.

“Mikumi kuna vipaji vingi vya muziki lakini hakuna aliyeweza kuviibua kwa miaka mingi, ila mimi nikiwa kama mbunge wao nitatekeleza ahadi hii kwa kuihamishia studio yangu Mikumi ili wasanii chipukizi waweze kufanya kazi zao”, alisema  Professor Jay.

Mwanalizombe ni studio inayomilikiwa na msanii huyo ambayo kwa sasa ipo maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es salaam na imeshatoa nyimbo kali kama Makamanda wimbo wa Sugu, Tatu Chafu na Kipi Sijasikia chini ya mtayarishaji Villy.

Leave your comment