EXCLUSIVE (TANZANIA) – Harmonize ajichora tattoo ya picha ya Diamond!
5 January 2016

Hitmaker wa single ya ‘Aiyola’ ambaye yupo chini ya label ya Wasafi Classic Baby (WCB) ameamua kuuthibitishia ulimwengu kuwa anajuvunia kuwa mtoto wa kimuziki wa staa wa Tanzania, Diamond Platnumz kwa kuchora tattoo yenye picha na kuandika jina la Simba.
Jina hilo la Simba lilizua utata kwa Mr Blue na kudai yeye ndiye alikuwa mwanzilishi wa jina hilo na Diamond ameiga tu.
Haya ndiyo maneno aliyoandika Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagarm;

“Katika Maisha Yangu Sikuwahi Kuwaza Kuwa Siku Nitajichora Tatoo Diamond Nimtu Mwenye Mchango Mkubwa Sanaa Katika Maisha Yangu Leo Hii Mimi Ninathaminika Kutoka Kwenye Kudhalaulika Nimekuwa Maarufu Na Kupata Uthamani Mkubwa Kupitia Yeye Siotu Kwa Kipaji Nilicho Nacho Kwani Wangapi Wana Vipaji…? Naisaidia Familia Yangu Kwa Kile Nikipatacho Sihaba Akiwa Na Mchango Wake Mkubwa Sana… Lakini Mwisho Wasiku Haya Ni Maisha Nahii Ni Dunia Inamambo Mengi Sanaa Hasa Sisi Vijana Ambao Niwepesi Wa Kujisahau Kinaweza Tokea Kitu Kidogo Sanaa Ukasahau Wema Na Fadhira Ulizotendewa, Lakini Pia Mungu Ndio Katukutanisha Na Karibia Watu Wengi Wanajua Tumekutanaje Kwamana Nimekuwa Nikiulizwa Katika Vyombo Vya Habari Tofauti Tofauti So Watu Wengi Wanajua Tulivyo Kutana But Hakuna Anaejua Tutaachana Vipi kwamana Sisi Ni Binadamu Kuna Kifo Leo Na Kesho Huwezi Jua Yawanadamu Ni Mengi Siamini Kuwa Binadamu Wote Duniani Wanafurahia Mahusiano Na Ukaribu Wetu Na Huwezi Shindana Na Binadamu Ukijua Yambele Wenzio Wanajua Ya Nyuma Ndio Mana Yakujichora Hiiii Picha Yake Ambayo Haitafutika Hadi Naingia Kaburini Hata ikitokea Hatupo Pamoja Nikiitazama Hii Picha Itabaki Kama Kumbu Kumbu Na Heshima Yangu Kwake Hadi Siku Yangu Ya Mwisho Haya Ni Maamuzi Yangu Binafsi..!”




Leave your comment