EXCLUSIVE (TANZANIA) – 2016 lawama kwa wasanii ziishe na tufanye kazi – Fella

 

Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe pamoja na TMK Wanaume Family, Said ‘Mkubwa’ Fella amewasihi wasanii kuutumia mwaka 2016 vizuri kwa kutoa kazi nzuri na kuacha malalamiko yasiyo na tija.

Fella ambaye ametambulisha kundi jipya liitwalo Salam TMK, alikiambia kipindi cha Enews cha EATV kuwa mwaka 2016 utakuwa mwaka mwema kama wasanii watautumia vizuri.

“Ninaweza kuwaambia wasanii wajibrand vizuri, lawama ndogo ndogo hazihitajiki tena mwaka 2016”, alisema.

“Kama kuna lawama zinahitajika basi ni za jumla au ziwe lawama kama mtu kaonewa au amenyanyaswa lakini tusilalamike ilimradi kugomea vitu wakati tunajua serikali yetu imeamua mpaka kutuwekea waziri ambaye atatusikiliza na kusikiliza matatizo yetu kwa maslahi yetu. Kwahiyo tunatakiwa kuwa wamoja na tutengeneze unity nzuri ili tufikie malengo yetu kwa pamoja”, alieleza zaidi.

Pia Said Fella ambaye ni diwani wa Kata ya Kilungule amewataka mashabiki wa muziki kuliunga mkono kundi la Salam TMK lililoachiwa wimbo wao wa kwanza wa ‘Nafsi’.

Leave your comment

Top stories