Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
EXCLUSIVE (TANZANIA) – Album ya Cinderella iliuza copy milioni 2 –Ali Kiba
13 November 2015

Staa wa muziki Tanzania King Kiba anayetamba na kibao cha ‘Chekecha Cheketua’ asema kuwa album yake ya kwanza ya Cinderella iliuza nakala milioni 2 (double platinum).
Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM alisema hajawahi kusikia rekodi hiyo kama imewahi kuvunjwa na msanii mwingine yoyote Tanzania.
“Kiukweli album yangu ya kwanza ya Cinderella ndiyo ilivunja rekodi na sijasikia mpaka leo rekodi hiyo imevunjwa” , alisema. “Sijui (nakala) ni milioni mbili vile, kitu kama hicho, kila album ilikuwa inauzwa mia mbili”, alisema Kiba.
Japo aliingiza zaidi ya milioni 200 King Kiba alisema utoto ulikuwa mwingi.
“Nilijenga kupitia album, vitu vingi nilifanya, yaani mpunga nilikuwa ninao alafu nilikua sijua kama ninao.Wewe unafikiri nilipumzika bure” aliongezea mwanamuziki huyo.
Weekly Top 10 songs

Black Mark utandilubi omwami wangu5:21
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Paver2:55
CHAMPION GAL3:00
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
BIkola2:58
The Prelude of Grace1:31
Joy Is Coming3:08
Worship My King5:00
Top stories
- Angel Prince Biography
27 May
- new song
26 May


Leave your comment