EXCLUSIVE (TANZANIA)- Kamikaze kuachia album ya rap hivi karibuni

 

 

 

Msanii Cyrill Kamikaze ametangaza kurudi kwenye aina ya muziki aliyokuwa akifanya awali (Rap) baada ya kutoa nyimbo za kawaida mfululizo kwa kipindi kirefu.

Aliongea na kipindi cha Bongo Fleva cha Clouds FM jumamosi iliyopita, Kamikaze amesema kutokana na maoni mengi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki wake ameamua kuja na album ya Rap itakayokuwa na nyimbo 13. Na pia aliongeza kuwa album hiyo itatoka hivi karibuni.

Kamikaze ambaye ameshawahi kutoa nyimbo za kawaida kama “Alowa” na “Nikikuona”, pia ametambulisha wimbo wake mpya wa Rap unaitwa “Bad news”

Katika ukurasa wake wa Instagram Kamikaze alipost picha siku ya jumamosi na kuandika “Tune in Clouds ! naachia single toka kwa Rap album…… kabla ya official single inayotoka soon pia.. #Singidaboy”.

Leave your comment