EXCLUSIVE (TANZANIA)- Video ya Ningefanyaje ya Ben Pol kufanyika Afrika Kusini -Justin Campos

 

 

 

Wasanii wengi wa Tanzania kwa sasa wamekuwa wakienda kushoot video za nyimbo zao nje ya nchi, kati ya directors wanaowatumia ni Justin Campos wa Afrka Kusini.Katika orodha ya wanamuziki hao sasa ameongezeka Ben Pol.

King huyo wa RnB ameamua kufunga safari kwenda Afrika Kusini kwaajili ya kushoot video ya wimbo wake mpya “Ningefanyaje” aliowashirikisha Anvril wa Kenya na msanii mpya Rosie M, ambayo amechagua kuifanya na director Justin Campos wa Gorilla Films.

Ni sababu ipi imemfanya kumchagua Campos; “Nimeamua kushoot na Campos kwasababu kiukweli haina ubishi Campos amefanya kazi nyingi nzuri sana na nyingi zina mafanikio. Na kuhusu kuuchagua ‘Ningefanyaje’ kuwa ndio wimbo wa kwanza kuufanyia video nje na director wa  nje. Mimi naiamini ‘Ningefanyaje’ sana na naamini kwamba kwa ubora wa video za Campos inaweza kwenda mbali zaidi” Ben Pol alisema.

Na aliongeza kuwa wanatarajia kuanza kushoot video hiyo Novemba 8 jumapili hii.

Wasanii wengine ambao wameshoot video Afrika Kusini ni pamoja na Vanessa Mdee (Never Ever), Aiyola ya Harmonize ambayo imetoka leo, Joh Makini (Don’t Bother) ft G Nako, Nikk wa Pili, Chege ft RunTown ambayo bado haijatoka (Sweet sweet) na wengine wengi.

Kutokana na kazi nzuri za wasanii wabongo wamefanikiwa kuweka headlines katika televisheni za kimataifa kama MTV Base, Trace Urban, SoundCity pamoja nazingine.

Leave your comment