EXCLUSIVE (TANZANIA)- Barnaba kufanya kolabo na msanii mwingine wa Uganda, Kleyah

 

Baada ya kufanya kolabo na Jose Chameleone wa Uganda, sasa Barnaba kufanya na msanii Kleyah kutoka huko huko.

Wasanii hao wanarecodi wimbo unaoitwa Msobe msobe katika studio za High Table Studio zinazomilikiwa na Barnaba.

Barnaba amesema “Kleya alinitafuta kupitia simu, alipewa namba yangu kupitia kituo kimoja hivi cha redio. Ni msanii ambaye mwenye uwezo mkubwa sana na sikutegemea msanii kama huyu angeweza kunitafuta maana nilimfatilia nikaangalia biography yake ipo vizuri, lakini aliniamini ndio mana tukafanya kazi. Nimemuimbisha Kiswahili humo ndani na ameimba vizuri”.

Mwanadada Kleyah ni msanii aliyezaliwa nchini Uganda na kusoma elimu yake ya juu katika maswala ya mawasiliano chuo cha Phoenix nchini Marekani. Kwa sasa Kleyah anaishi Tanzania anatarajia kumaliza elimu yake ya utawala wa kimataifa ( Degree in International Management).

Pia msanii huyo mbali na kusoma yupo nchini chini ya usimamizi wa mkufunzi wa sauti, Luigi Tamburi na Mzungu Kichaa. Kati ya kazi zake ni “Lovers Eyes” na “Don’t Sly Me” zilizotayarishwa na Ogopa Deejays wa Kenya.

source: Bongo 5

Leave your comment