Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
"Hits Only" Diamond Athibitisha Collabo Yake Na Darassa Iko Mbioni
21 February 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye, msanii Darassa amedokeza kuwa yuko mbioni kuachia collabo na msanii kutokea lebo ya WCB, Diamond Platnumz.
Darassa ambaye aliupamba mwaka 2023 na hits zake mbili ambazo ni Nobody akiwa na Bien pamoja na I Don't Care amedokeza ujio wa collabo hiyo ambayo mashabiki wamekuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa alichapisha video ambayo inamuonesha akiwa na Diamond Platnumz na kuandika:
“WCB Big Boss Diamond Platnumz ametoa go ahead sasa mabibi na mabwana boys and girls tukutane hapa 22nd”
Diamond alijibu chapisho kwa kuandika “HITS ONLY” kauli iliyothibitisha kuwa huenda wawili hao wanaachia mkwaju wao wa pamoja tarehe 22 mwezi February.
Weekly Top 10 songs

Fanta0:00
CHAMPION GAL3:00
Tudo Trocado3:17
ONLY YOU JESUS5:44
Joy Is Coming3:08
Nasema3:02
Minha Historia3:41
BESTIE2:26
Akaana kokukyalo2:21
Baraka4:33
Top stories
- Baamane
04 July
- Listen To Me Please
04 July


Leave your comment