Q Chief Adokeza Ali Kiba Kuja Na Redio Yake Hivi Karibuni

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Legend wa muziki wa Bongo Fleva, Q Chief hivi karibuni amedokeza kuwa CEO wa Kings Music, Ali Kiba yuko mbioni kufungua chombo chake cha habari yaani redio na TV. 

Q Chief alidokeza kuhusu ujio wa chombo hicho cha habari kutoka kwa Ali Kiba ikiwa ni wiki chache tangu wanamitandao na bloggers kutoka Tanzania kudokeza kuwa Ali Kiba na Joseph Kusaga ambaye ni mmiliki wa Clouds Media wameungana pamoja kufungua kituo kipya cha redio. 

Kwenye ujumbe mrefu ambao Q Chief aliuandika kwenye ukurasa wake Instagram alisema kuwa Ali Kiba anatarajiwa kuja na kituo chake cha habari kama ambavyo Diamond anamiliki Wasafi Media na katika ujumbe wake huo   alimuonya Diamond kwa kile alichokiita “uonevu” dhidi yake. 

“Jiandae Ali Kiba anakuja na media yake sidhani kama atakuwa na mfumo uonevu kama wako” aliandika Q Chief 

Ujumbe huo kutoka kwa Q Chief umezua taharuki kwenye kiwanda cha muziki Tanzania huku wengi wakiwa wanajiuliza ni nini hhasa kimetokea baina yake ya Diamond. 

Ikumbukwe kuwa Diamond Platnumz ni sehemu ya wamiliki ya Wasafi FM na Wasafi TV akiwa ni mmoja ya wasanii wachache Afrika ambao pia ni wamiliki wa vyombo vya habari. 

 

Leave your comment