Director Kenny Afichua Sababu Ya Kuacha Kufanya Kazi Na Diamond Platnumz

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Muongozaji wa video za muziki maarufu kutoka nchini Tanzania, Director Kenny hivi karibuni amedokeza sababu za kuacha kufanya kazi na msanii Diamond Platnumz. 

Director Kenny alianza kujijengea jina lake mwaka 2018 baada ya kuanza kutayarisha video za wasanii wa WCB Wasafi.

Kenny ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Hanscana kabla ya kuwa maarufu, kipindi yuko Wasafi alihusika kutayarisha video kali za Bongo Fleva kama Kwangaru, Nisamehe, Saula, Dede na Yope Remix ya Diamond Platnumz pamoja na Innos B ambayo ndio video ya muziki kutoka Afrika Mashariki iliyotazamwa zaidi YouTube. 

 

Akizungumza kwenye mahojiano kwenye kipindi cha XXL, Kenny alidokeza kuwa aliacha kufanya kazi na Diamond kutokana na sababu za kibiashara, kwani yeye  alikuwa anataka aanzishe kampuni yake mwenyewe ya kutayarisha video badala ya kuwa nchini ya Zoom Extra ambayo ilikuwa ni kampuni ya Diamond Platnumz. 

 

“Mwenyewe kama Director Kenny niliamua nifungue kitu changu kwa hiyo, hiyo ndo ilikuwa sababu (ya kuondoka). Nilitaka kufungua kitu changu mwenyewe” alizungumza Kenny ambaye kwa sasa ni CEO wa kampuni ya DK company. 

Aidha katika mahojiano hayo, Kenny alidokeza kuwa, yupo tayari kufanya kazi tena kazi na Diamond iwapo itatokea nafasi ya kufanya hivyo. 

 

Leave your comment