Rapa Country Wizzy Afichua Ngoma Yake Bora Ya Muda Wote

By Charles Maganga

Siku chache tangu rapa kutokea lebo ya Bxtra Records, Country Wizzy hivi karibuni amefichua ngoma yake bora ya muda wote tangu aanze muziki. 

 

Country Wizzy ambaye kwa sasa yuko nchini ya lebo ya Bxtra Records, amedokeza kuhusu ngoma hiyo kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni. 

 

Tangu aanze muziki miaka 13 iliyopita kufika sasa Country ameshaachia ngoma takriban 59 ikiwemo album moja ya kuitwa Yule Boy ambayo iliingia sokoni mnamo mwaka 2019. 

 

Akizungumza kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, Wizzy alidokeza kuwa ngoma yake ya Zee La Kukomesha ni moja kati ya ngoma zake bora alizowahi kuzifanya na hii ni kutokana na namna ambavyo kwenye ngoma hiyo aliweza kuelezea maisha yake tangu alipoanza mpaka sasa. 

 

“Zee La Kukomesha ni ngoma yangu bora ya muda wote na ilibadilisha kabisa maisha yangu ya muziki. Ngoma inaelezea wapi nilipotokea kwani watu walikuwa hawamiani kipindi naanza.” Akizungumza Wizzy kwenye mahojiano hayo. 

 

Kwa sasa Wizzy anatamba na video yake ya Current Situation ambayo inafanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. 

 

Leave your comment