Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Nandy Afunguka Kuhusu Collabo Na Usher Raymond
19 February 2024
By Charles Maganga
Msanii kutokea nchini Tanzania, Nandy hivi karibuni amefungua kuhusu collabo yake na msanii kutokea nchini Marekani, Usher Raymond.
Nandy ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Dah! siku chache zilizopita alitumia akaunti yake ya Instagram alichapisha mazungumzo yake na msanii wa nchini Marekani, Usher ambapo kupitia mazungumzo hayo, Usher alidokeza kuwa tuko tayari kufanya remix ya ngoma ya Dah!
Ikumbukwe kuwa Usher kwa sasa ni moja ya wasanii wanaofanya vizuri sana duniani na hii ni baada ya kutumbuiza kwenye Yukio la Superbowl nchini Marekani pamoja na kuachia albamu yake ya kuitwa Coming Home.
Akizungumza kuhusu collabo hiyo, Nandy wakati anahojiwa na waandishi amedokeza kuwa kwa sasa mashabiki zake inabidi wasubiri collabo hiyo.
Mara collabo hiyo itakapotoka, Nandy atajingia kwenye orodha ya wasanii kutoka Tanzania ambao wameshawahi kufanya collabo na wasanii kutoka Marekani. Wasanii wengine ni pamoja na Diamond Platnumz, AY pamoja na Harmonize.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Playlist my upcoming song
30 March
- ITSLILREMY
30 March
- Usman Khalifa Amoto
30 March
- Ingopangani Download nyimbozi
30 March




Leave your comment