Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Iyanya Kuungana Na Ali Kiba Kwenye "Huku Remix"
17 February 2024
By Charles Maganga

Bila shaka msanii kutoka nchini Nigeria, Iyanya yuko mbioni kufanya kazi na msanii kutokea nchini Tanzania na CEO wa Kings Music Ali Kiba.
Siku chache zilizopita Iyanya alitua nchini Tanzania ili aweze kuitangaza album yake mpya ya Once Upon A Cat ambayo imetoka hivi karibuni.
Kwenye ukurasa wa Instagram wa Kings Music, label hiyo ilipost video fupi inayomuonesha Ali Kiba akiwa na Iyanya studio pamoja na producer Abbah ambapo wakati wanarekodi ngoma ya Huku ilikuwa ikisikika.
Video hiyo kutoka kwenye ukurasa wa Kings Music ilisindikizwa na ujumbe usemao “Huku Studio Session With Iyanya Ni Noma Sana. Abbah Process malizia nyimbo nitoke baba”
Kwa collabo hii, Ali Kiba anatarajiwa kuwa msanii wa pili kufanya kazi na Iyanya baada ya Diamond Platnumz ambaye takriban miaka 10 nyuma alishafanya kazi na Iyanya kwenye Bum Bum na Nakupenda
Weekly Top 10 songs

Inama4:58
ONLY YOU JESUS5:44
Bikyaganye3:29
Mshamba2:44
Daddy2:50
Sissa3:37
Eazzy Ft Way Dee2:59
Alaska2:29
Older (Drill Remix)2:06
LOCATION2:11
Top stories
- Music updates
05 October
- Have you joined the Kachumbali Army yet?
05 October
- Have you tasted some Kachumbali today
05 October



Leave your comment