Baddest 47 Arudi Kivingine Na Ngoma Mpya "Mapenzi"

By Charles Maganga 

Baddest 47, moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania kwa mara nyingine ameamua kuburudisha mashabiki baada ya kuachia Mkwaju mpya wa kuitwa Mapenzi 

 

Ngoma ya Mapenzi kutoka kwa Baddest 47 inakuja miezi michache tangu Mshindi huyo wa tuzo za TMA kuachia ngoma zake mbili mwaka jana ambazo ni Kampito pamoja na Miluzi

Kwenye Mapenzi, Baddest 47 anachanganya Bongo Fleva na Amapiano ambapo katika ngoma hii Baddest anatumia lugha ya ubunifu kuelezea namna ambavyo mahusiano yanaweza yakamuumiza mtu au kumuweka kwenye hali ya furaha. 

 

Baddest ni msanii kutoka Tanzania baye anajulikana kwa ngoma zake kama Zagamua, Nikagongee na nyinginezo nyingi. 

Sikiliza Mapenzi By Baddest 47 Hapa: 

https://www.youtube.com/watch?v=uFAHPhShgfk

Leave your comment