Ngoma 5 za Mapenzi za Kusikiliza Msimu Huu wa Valentine

Image: Online

Writer: Charles Maganga

 Download New Kalenjin Dj Mixes on Mdundo

Ukweli ni kwamba Valentine ni moja ya siku pendwa hasa kwa watu wanaopendana na kwa hapa nchini Tanzania, siku hii hupambwa na zawadi kedekede baina ya wapenzi, mitoko baina ya wapendanao na kubwa kabisa muziki mzuri ambao hupambwa siku hii.

Kwa kulifahamu, wasanii kutoka Tanzania wamekuwa mstari wa mbele kutengeneza ngoma ambazo bila shaka zitaweza kupamba msimu wa Valentine.

Kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma 5 kutoka ambazo unatakiwa kusikiliza kwenye msimu huu wa Valentine:

Daah - Nandy

Kama unatafuta ngoma mahususi kwa ajili ya kumtumia mwenza wako basi Dah! ya Nandy ni chaguo sahihi. Ngoma hii iliyotayarishwa na S2kizzy na kupambwa na sauti ya “The African Princess” yaani Nandy bila shaka itapamba Valentine yako mwaka huu.

https://youtu.be/Oio_zNm9rxM?si=aLZuKu7sEqhFfiUw

 

Mapoz - Diamond Platnumz Ft Jay Melody & Mr Blue

Mkwaju huu ambao umetokana na ngoma ya miaka ya 2000 bila shaka si ngoma ya kukosa kwenye playlist yako ya Valentine mwaka huu. Hii ni ngoma ambayo unaweza ukasikiliza ukiwa kwenye chakula cha usiku wa Valentine au ukiwa kwenye mtoko usiku wa leo.

https://youtu.be/M1dUTxVXS5Q?si=HE9aAYw9BtTQ7sb9

 

 Zawadi - Zuchu

Zuchu ni hodari wa kuandika ngoma za mapenzi. Uhodari huo alianza kuuonesha  kwenye kwenye Wana, Utaniua na kwenye Valentine hii ameachia ngoma ya Zawadi ambayo ni maalum kwa ajili ya wapendanao.

https://youtu.be/nqxrYkKei0E?si=S38F4CVpXNceAyN-

 

 Umechelewa - Mbosso

Ufundi wa kuandika aliounesha Mbosso kwenye Umechelewa ni kigezo Tisha cha kufanya ngoma hii iwe ni wimbo wako wa Valentine. Mpangilio mzuri wa sauti, mashairi ya aina yake pamoja na maudhui mzima ya ngoma hii ni wazi kuwa ni maalum kwa watu wanaopendana.

https://youtu.be/zUiRTc7v-X4?si=Wti0idc02ANZMT4D

 

Away - Marioo Ft Harmonize

Kwa wapenzi wa Bongo Fleva, Away bila shaka itasimama kama chaguo bora kwao hasa ukizingatia kwamba kwenye ngoma hii ya mapenzi, Marioo ametumia sauti yake kufikisha ujumbe kwa mpenzi wakati Harmonize ametumia ufundi wake wa kuandika mistari kupamba ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=Ux9wMQ4x8RE

 

 

 

 

 

 

Leave your comment