Usher Aiomba Remix Daah! Kutoka Kwa Nandy

Picha: [Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Mwaka huu pengine unaweza kuwa mwaka mzuri zaidi kwa Mmiliki la lebo ya African princes Nandy na hii nikutokana na matokeo ya  kibao chake kipya anachotamba nacho kwa sasa alichokipa jina la Daah!

 

Suala hili limedhihirika masaa machache baada ya mwanamziki huyo kuweka wazi jumbe fupi kupitia ukurasa wake wa Instagram zikionesha msanii kutokea Marekani Usher akihitaji kuifanyia ngoma hiyo remix na kuzua taharuki kubwa.

 

Upepo huu kwa Nandy unaweza kuwa neema hata kwa wasanii wengine licha ya kuwa baadhi ya wanamitandao wemependekeza kuwa ingekuwa vyema kama angetoa taarifa hizo mara baada ya ushirikiano huo kukamilika kwanza.

Download Bongo Mapenzi Mix For Free on Mdundo.com


Wimbo wa Daah! Ni ngoma ambayo Nandy amefanikiwa kuitoa katika awamu mbili ambayo ya kwanza aliifanya mwenyewe huku awamu ya pili akiitolea video ambayo amemshirikisha msanii nguli kutokea lebo ya Kingz music Alikiba.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii kutokea Tanzania kufanya ngoma na wanamzuki wakubwa duniani ikumbukwe pia mwaka 2021 Rayvanny alilamba shavu katika wimbo wake wa Tetema remix alioufanyia remix na Maluma ambao pia umefanya vizuri na kufungua milango zaidi kwa Vannyboy

 

https://www.youtube.com/watch?v=Oio_zNm9rxM

Leave your comment