Jaiva Kuachia Video Ya buruda

Picha: [Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Mwanamuziki anayetamba na kibao chake cha Buruda Jaiva amethibitisha kuachia video ya ya ngoma yake hiyo ambayo amemshirikisha mwanamuziki Marioo.

 

Listen To Amapiano Mix For Free on Mdundo.com

Uthibitisho huo Jaiva ameutoa wakati alilofanya mahojiana na Sky Bundala huku akieleza ya kuwa video hiyo itafanywa na Director chipukizi akisaidiana na moja kati ya director wakongwe nchini.

 

Ushirikiano huo wa director katika video ya Buruda, Jaiva amesema ni katika hatua ya kutoa nafasi zaidi kwa waongizaji wa Muziki chipukizi katika kuonesha uwezo wao na ukubwa wa kazi zao za ubunifu katika video za muziki.

Mbali na kuongelea kuhusiana na wimbo wa Buruda lakini pia msanii huyo mwenye sauti yenye upekee wa aina yake ameufahamisha UMMA ya kuwa wimbo wake wa SOUP alilofanya na Marioo ndiyo ngoma ambayo imemfanya aweze kusikiaka zaidi katika maisha yake ya Muziki.

 

Katika mahojiana hayo yaliyokuwa na sehemu mbili pia Jaiva pia aliweka wazi upande wake na suala la Chinno kutokana na mtafariko uliojitokeza kati yake pamoja na Marioo, huku pia akimtaka msanii huyo aweze kuondoka utata huo kati yao.

Kwa sasa Jaiva Yuko chini ya Bxtra iliyo chini ya Hammy B na pia msanii huyo ameweza kuelezea ukaribu wake na Hammy kuwa ni zaidi ya kazi na kuonesha kupendezwa na suala hiyo katika muziki wake.

https://www.youtube.com/watch?v=uXG8gKvMt38

Leave your comment