Diamond Platnumz Aachia Video ya Mapozi

Picha [Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Mwanamuziki na Mmiliki wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platnumz ameachia video ya ngoma yake Mapozi aliyomshirikisha Mr blue pamoja na Jay Melody.

Pakua Love Songs Bure Kupitia Mdundo.com

Mapozi ni ngoma iliyopita katika mikono ya Director Ivan na kuitendea haki ilivyo vyema kwa ubunifu na mpangilio wa mandhali katika video hiyo.

Ikumbukwe ya kuwa kabla ya Mapozi kuachiliwa miaka takribani 14 iliyopita Mr blue aliachia ngoma hiyo ikiwa ndiyo ngoma halisi kabla ya kurudiwa tena mwaka huu.

Katika video hiyo uhalisia wa ukale umeonekana katika mavazi ambayo yametumika yakiwa yamebeba maudhui ya ukale kama ngoma yenye. Kuanzia nguo mpaka bandeji usoni na bila kusahau namna ya uchezaji katika video hiyo wenye madoido ya aina yake. Kitendo hichi kimefanya wimbo huo usipoteze ladha yake tangu kuachiliwa kwake miaka zaidi ya kumi iliyopita.

Kwa sasa ni masaa machache pekee tangu kuachiwa kwa ngoma hiyo na katika kuonesha ukubwa wake tayar Mapozi imeingia katika ngoma zinazotazamwa zaidi YouTube ikiwa na zaidi ya watazamaji lakin mbili.

Ni zaidi ya miezi mitatu tangu Simba aachue video na kwa mwaka 2024 hii ni video ya kwanza ambayo Diamond kuachia tangu mwaka uanze. Hivyo mengi zaidi yanatarajiwa hasa kutokana na kasi ya utoaji  wa video kutoka kwa Diamond Platnumz.

 

https://www.youtube.com/watch?v=M1dUTxVXS5Q

Leave your comment