Amrouche Atimuliwa Taifa Stars - AFCON

Picha [AFCON 2023/Ghanaian Times]

Mwandishi : Pharis Kinyua

Wakati timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ikiendelea kuuguza kidonda cha bao 3 - 0 dhidi ya Morocco walichopata  katika michuano ya AFCON, Shirikisho wa soka la Tanzania TFF limemsimamisha kazi kocha mkuu wa timu hiyo Adel Amrouche.

 

Hatua hiyo imejiri siku chache kupita baada kocha huyo kutoa kauli zilizoleta utata na kupelekea Shirikisho la soka la nchini Morocco kupeleka malalamiko yao katika kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka barani Africa (CAF) juu ya kauli hizo zilizoipa taswira mbaya CAF.

Amrouche mwenye miaka 58 aliituhumu Morocco kuwa na ushawishi juu ya upangaji wa waamuzi pamoja na matokeo katika mechi zake na kufanya CAF kuonekana kama vibaraka wa Morocco.

Download Baikoko Bongo Mix on Mdundo For Free

Mbali na hatua hiyo pia Shirikisho hilo la soka barani Afrika limemsimamisha kocha huyo ambaye pia ana asili ya Algeria katika mechi nane mfululizo.

Baada ya uamuzi huo Shirikisho la soka nchini Tanzania  limemteua  Hemed Morocco kuwa kaimu kocha wa Taifa Stars  ambaye pia atasaidiana na kocha Juma Mgunda katika kuinoa Taifa Stars katika kipindi hiki.

 

Kwa sasa katika kundi F walilopo Taifa Star wamebakiza mechi 2 pekee ambazo watacheza na DRC Kongo pamoja na Zambia ingawa katika kundi hilo Taifa Stars wanashilikia mkia wakiwa hawana alama yoyote.

Leave your comment