Taifa Stars Yala Kichapo Cha 3-0 Dhidi Ya Morocco

Picha [Morocco World News]

Saa chache zilizopita Tanzània iligubikwa na huzuni baada ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, kufungwa bao 3-0 katika mechi yao ya ufunguzi kwenye michuano ya AFCON 2023,

 

Taifa Stars ambayo kwa wachambuzi wengi inatazamwa kama timu dhaifu mbele ya Morocco bila shaka walikuwa na mengi ya kuthibitisha kwenye mechi hiyo ambayo ilichezwa majira ya saa 2 muda wa Afrika Mashariki. 

Listen To Kaswida Mpya For Free on Mdundo 

Morocco ilifungua mlango wa ushindi kupitia bao la Saiss katika kipindi cha kwanza cha mchezo na mpaka wanaingia kwenye mapumziko, Morocco, timu ambayo pia iliweza kufuzu nusu fainali kwenye michuano ya Kombe La Dunia 2022 ilikuwa ikiongoza kwa goli 1-0

 

Timu hiyo ya Kaskazini mwa Afrika iliongeza goli la pili katika dakika ya 77 ya mchezo na En-Nesyri alidunga bao la tatu dakika tatu baadaye yaani dakika ya 80.

 

Katika mchezo huo pia Taifa Stars ilikutana na pigo la aina yake baada ya  Novatus Miroshi kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 70 hivyo kupelekea Tanzania kumaliza mchezo huo na wachezaji kumi.

 

Kwa sasa Taifa ambao wako kwenye kundi F, wanashika mkia katika kundi hilo huku Morocco wakiwa wanaongoza.  Washiriki wengine katika kundi hilo ni Zambia na DRC ambao baada waliopata droo ya 1-1 kwenye mchezo wa jana.

Leave your comment