Stephen Aziz Ki na Wachezaji Wengine 6 Kutoka Yanga Ambao Wanashiriki AFCON 2023

Picha [Instagram/Yanga]

Tasnia ya mpira wa miguu barani Afrika kwa sasa bila shaka imeelekeza macho yake yote katika michuano ya AFCON na Yanga ikiwa moja ya timu kubwa hapa Tanzania imeweza kupelekea baadhi ya wachezaji wake kwenye michuano hiyo ya kukatana shoka.

 

Listen To Yanga Mabingwa By Marioo on Mdundo

Yanga SC, ambayo ni mabingwa mara 49 wa michuano ya NBC Premier League Tanzania, inajivunia kuwa na wachezaji 7 wanaoshiriki katika AFCON, wachezaji hao wakiwa wanawakilisha timu zao za Taifa kama Burkina Faso, Tanzania, na Zambia.

 

Baadhi ya wachezaji wa Yanga wanaong'ara katika AFCON 2023 ni pamoja na Djigui Diarra kutoka Mali, Stephen Aziz Ki kutoka Burkina Faso, Kennedy Musonda kutoka Zambia, Ibrahim Abdullah kutoka Tanzania, Mudathir Yahya Abbas kutoka Tanzania, Bakari Nondo Mwamnyeto kutoka Tanzania, na Dicksoni Job kutoka Tanzania

 

Ikumbukwe kuwa kwa sasa Yanga inaendelea na mazoezi ya kujinoa Kwa ajili ya maandalizi ya Kombe La FA pamoja na NBC Premier League ambayo inatarajiwa kuanza muda si mrefu kuanzia sasa.

Leave your comment