Real Madrid Mabingwa Spanish Super Cup

 

[Picha/ Chanel Television]

Usiku wa Januari 15 2024, ulishuhudiwa mtanange wa kukata na shoka mara baada ya Real Madrid kuvaana na Barcelona katika fainali za Spanish Super cup zilizofanyika katika uwanja wa Al Awwal huko Saudi Arabia.

Katika mtanange huo wa aina yake Madrid alishuhudiwa akiondoka na ubingwa wa kombe hilo baada ya kumpatia kichapo Barcelona cha bao 4-1.

Sambamba na ushindi huo winga kutokea Los Blancos, Vinicius Jr aling’ara zaidi na hii ni baada ya kufunga hattrick katika fainali hizo,  Huku magoli yote matatu yakipatikana katika kipindi cha kwanza cha mchezo. Naye winga wa kushoto  Rodrigo alimalizia ushindi huo kwa bao Moja lililotamatisha ubingwa wa Madrid.

Download Singeli Mpya For Free on Mdundo 

Bao la kifutia machozi kwa Barcelona lilifungwa na mshambuliaji wa zamani kutokea Bayern Munich, Robert Lewandowski katika dakika ya 33 baada ya mchezo huo kuanza.

Ushindi huu wa 13 kwa Madrid ni kisasi kwa Barcelona baada ya msimu uliopita Barcelona kuwaacha Madrid na majonzi katika fainali hizo baada ya kuondoka na ubingwa wa magoli 

Licha ya kupoteza ubingwa huo ikumbukwe ya kuwa bado Barca anaongoza kwa kuwa na vikombe 14 vya Super cup akifualiwa na hasimu wake Madrid kwa kuwa na jumla ya viko 13 baada ya ushindi huu.

Leave your comment