Ufunguzi AFCON 2024 - Hatua Ya Makundi

Picha [Daily News]

Michuano ya kombe la mataifa Africa kwa msimu wa mwa 2023/ 2024 imeanza kutimua vumbia Jumamosi hii katika viwanja tofauti nchini Ivory Coast.

Katika michuano hiyo inayounganisha timu 24 kutokea barani Africa kwa sasa iko katika hatua ya makundi yenye kundi A mpaka kundi F huku kila kundi likiwa na timu nne.

Wenyeji wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Ivory Coast walianza vyema katika kundi lao mara baada ya kuondoka na ushindi wa bao 2 kwa 0 dhidi ya timu ya Taifa ya Guinea.

Mbali na mchezo huo mechi zingine zilizochezwa siku ya ufunguzi ni pamoja na Ile mechi iliyoihusisha timu ya Taifa ya Ghana ambazo wao waliambulia kuchapo cha bao 2 dhidi ya Timu ya Taifa ya Cape Verde.

Download Nyimbo Mpya For Free on Mdundo

Me hi zingine zilizochezwa siku hiyo ni pamoja na Timu ya Taifa ya Misri dhidi ya Msumbijia iliyoisha kwa sare ya bao 2 l, huku nao Nigeria wakimaliza mechi Yao ya kwanza kwa sare ya bao moja dhidi ya Equatorial Guinea.

Mbali na mechi hizo zilizoanzan huko AFCON lakini pia wasanii mbalimbali walitumbuiza katika ufunguzi wa michuano hiyo kutokea barani Africa.
Wasanii hao ni kama vile Magic system kutokea nchini Ivory Coast ,Yemi Alade wa Nigeria pamoja na Mohamed Ramadan kutokea Misri.

 

Leave your comment