Nyimbo 5 bora Tanzania 2023

Mwaka 2023 umekuwa mwaka bora sana katika kiwanda cha Muziki wa Tanzania kutokana na umahiri uliofanywa na wasanii wake katika utoaji wa kazi zenye mvuto na umaridadi kwa ndani na nje ya nchi. 

Kwa mwaka huo wasanii walifanikiwa kushuhudia kazi zao zikizaa matunda kwa mashabiko wao ambazo walionesha kupendezwa na kazi hizo, na zifuatazo ni baadhi ya ngoma zilizofanya vizuri kutokea Tanzania kwa mwaka 2023.

5. No body - Darasa Ft Bien Baraza

Moja kati wa wasanii wa Rap kutokea Tanzania ambazo hufaamika kwa ‘Come back’ zenye kukonga moyo ni Darasa CMG. Katika ngoma hii ya mahaba, Darasa amezidi kuuthibitishia Umma wa sana juu ya umahiri wa andishi wake na awamu hii akivuka mipaka hadi nchini Kenya na kuungana na Bien.

4. Nitasema - Jay Melody

Kama moja ya wasanii waliozidi kujikita na Bongo Fleva, Jay Melody amaezidi kuzikosha nyoyo za mashabiki zake ambao wengi wao wakiwa ni wanawake. Uhodari wa uandishi wake katika ngoma kumemfanya awe moja ya wasanii wasio isha mvuto katika aina hiyo ya uandishi.

Download Nitasema For Free on Mdundo

 

3. Enjoy - Jux ft Diamond Platnumz

Moja kati ya nyimbo zenye kujaa ushehereshaji ni pamoja na wimbo huu wa Enjoy. Licha ya kuwa ni baadhi ya ngoma zenye watazamaji wengi huko YouTube lakini pia ni wimbo uliofanikiwa kuteka masikio ya mashabiki wa Muziki burudani. 

2. Single Again - Harmonize

Katika ngoma zilizomfanya Harmonize azidi kuonekana bora zaidi ni single again.
Wimbo huu ulijizolea umaarufu haswa mara baada ya kueleza story ya aliyekuwa mpenzi wake, Kajala. Harmonize bado amezidi kuonesha makali yake katika midundo ya Amapiano.

Download Darasa Music For Free on Mdundo

1. Shu! - Diamond ft Chley 

Moja kwa Moja mpaka Afrika ya Kusini ambapo Diamond Platnumz alipomshirikisha Chley katika Amapiano.
Ngoma hii imezua umaarufu haswa mara baada ya muda mfupi tu tangu kuachiliwa kwake.

Leave your comment