AWAY BY MARIOO FT HARMONIZE (REVIEW) 

 

Baada ya kufanya kazi na Ali Kiba, Abigail Chams, Mocco Genius na wakali wengine wakubwa mwaka jana, msanii Marioo ameuanza mwaka 2024 kwa kishindo baada ya kuachia collabo yake mpya na Harmonize ya kuitwa Away. 

 

Away ni collabo ya pili kati ya Marioo na Harmonize baada ya wawili hao kukutana kwenye Naogopa, ngoma iliyoachiwa mwaka 2022 huku video yake ikiwa imeweka rekodi ya kuwa video ya pili ya muziki kutoka Tanzania kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa mwaka 2023. 

 

Download Marioo Music For Free on Mdundo

Away ni ngoma yenye mahadhi ya Bongo Flava na ndani yake Marioo na Harmonize wanaimba kuhusu mapenzi ambapo wawili hao wanawaimbia wapenzi wao huku wakiwahasa wasiondoke kwenye maisha yao. 

 

Ngoma hii bila shaka itakuwa ni chaguo la wengi hasa wapendanao pindi wakiwa kwenye mapumziko yao ya kawaida, wakiwa vacation au hata kupigwa kwenye sherehe. Ndani ya Away utapenda namna ambavyo Marioo amepamba kibao hiki kwala sauti yake tulivu pamoja na Harmonize ambaye ametendea haki ngoma kwa mashahiri pamoja na midondoko yake ambayo imevutia wengi. 

 

Away imetayarishwa na mtayarishaji wa muziki kutokea Tanzania wa kuitwa Sky huku maandalizi ya mwisho yaani mixing mastering yakishughulikwa na Cukie Dady.

Leave your comment