Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
HUU MWAKA REMIX BY DAYOO FT RAYVANNY (REVIEW)
13 January 2024

Moja kati ya ngoma zinazofanya vizuri kwa sasa kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki ni pamoja na huu mwaka ya kwake Dayoo akiwa na gwiji kutokea Next Level Music, Rayvanny .
Mwaka huu remix ambayo Rayvanny ameshirikishwa na Dayoo imekuja takribani siku 10 tangu toleo la kwanza la ngoma hiyo kuachiwa tarehe Januari Mosi, 2024.
Kwenye Mwaka Huu Remix, Rayvanny anafungua verse ya kwanza ya ngoma hii kwa kukumbushia maisha yake ya zamani na kuapa kwamba mwaka huu atafanya mambo mazuri zaidi huku Dayoo akipamba ngoma hii na chorus kali ambayo bila shaka itaenda kuwa kivutio kwa watumiaji wa mtandao wa TikTok.
Download Dayoo Music For Free on Mdundo
Mwaka Huu Remix ni ngoma yenye mahadhi ya Bongo Piano yaani muunganiko wa Bongo Flava na Amapiano, aina ya muziki ambayo ina asili kutokea Afrika Kusini.
Video ya Huu Mwaka Remix imetayarishwa na Director Chris ambaye ameshafanya kazi na wasanii Tofauti Tofauti kutoka Tanzania ikiwemo Nandy, Billnass, Yammi na wengineo wengi.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- JORO STARR
31 March
- Kaká boye
01 April
- NEW MANAGEMENT
01 April




Leave your comment