Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Kwa washirika Wetu Kwa Kuwezesha Shughuli Ya Saba Saba : Tunasema Asante!
19 July 2023

[Image Source: Mdundo.com]
Pakua Mixes Mpya Kila Siku Ndani Ya Mdundo
Kwa heshima na furaha kubwa, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa washirika wetu wa Mdundo.com kwa kufanikishia shughuli ya Saba Saba mjini Dar es Salaam.
Tungependa pia kuwashukuru washirika wengine kama vile Koncept Media, Rick Media, Bongo 5, Simulizi na Sauti, Yinga Media, Clouds Media, Bekaboy Media, Citimuzik Media, na Vodacom Tanzania kwa ushiriki wao wa dhati katika kufanikisha tukio hili.
Ushirikiano wenu uliwezesha kuleta pamoja wadau mbalimbali na kutoa jukwaa zuri la kushirikishana uzoefu, maarifa, na mawazo katika sekta ya burudani. Pamoja na jitihada zetu, tumefanikiwa kufanya tukio la Saba Saba kuwa la kuvutia, la kufanikiwa, na lenye heshima kubwa katika jamii. Hata hivyo tulifurahia uwepo wa mashabikli wetu kwenye banda la Vodacom na hata pia tuliona uwepo wa aliyekua rais wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete akihudhuria shughuli ya Saba Saba. Hii inaonyesha dhamira ya viongozi katika kuimarisha sekta ya uchumi na biashara ya Wananchi wa Tanzania.
Tunaamini ushirikiano huu utaendelea kuimarisha sekta ya burudani na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya tasnia yetu. Tunathamini sana juhudi zenu, na tunatarajia kushirikiana nanyi tena katika matukio mengine ya baadaye.
Tena, tunawashukuru sana kwa moyo wa dhati kwa kila mmoja wenu kwa kuwezesha mafanikio ya shughuli hii ya Saba Saba.
Weekly Top 10 songs

Kamwambie3:47
chile-one-so-lucky4:02
Joy Is Coming3:08
TUMWAMBIE MUNGU ASANTE0:49
Malaika2:49
NALOKINGA2:52
Stima - Buruklyn Boyz5:04
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
Buwooma2:44
Alifata Hela3:53
Top stories
- NEW MANAGEMENT
01 April
- Love
01 April
- My biography
02 April
- STREAM NEXARITO SONGS ON SPOTIFY
02 April


Leave your comment