Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Ngoma Mpya : Gnako Atangaza Kufanya Kaz Na Wasanii Bongo
25 May 2023

Picha: Facebook
mwandishi:Charles Maganga
Rapa kutoka Bongo G Nako, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo “Shuga Daddy” ambao ameshrikiana na Juma Jux, hivi karibuni ametangaza kwamba yuko mbioni kuachia ngoma mpya ambayo ameshirikisha wasanii watatu wakubwa kutoka Tanzania
Rapa huyo ambaye pia ni mshiriki kwenye kundi la Weusi ameweka wazi kwamba hivi karibuni ataachia collabo akiwa ameshirikisha wasanii wakubwa. G Nako ni rapa maarufu Tanzania ambaye ametamba na ngoma kama “Gusanisha” “Original” na nyinginezo nyingi
Akiwa kwenye mahojiano hivi karibuni, G Nako amedokeza kwamba tayari ana ngoma ambayo ndani yake amemshrikisha Whozu, Juma Jux na Jay Melody
“Kuna (ngoma) nyingine inakuja. Yuko Whozu, kuna Jay Melody, niko mimi alafu yuko Jux” alizungumza G Nako kwenye mahojiano na XXL.
G Nako sio mgeni kwenye uwanja mzima wa collabo. Kufikia sasa rapa huyo ameshashirikiana na wasanii wengine wengine kutoka Tanzania ikiwemo Vanessa Mdee, Shetta, Ben Pol, Maua Sama na wengineo wengi.
Weekly Top 10 songs

Hatuachani8:47
Every push.2:01
Blessings Flow2:26
PENDEZESHA0:35
Daddy2:50
Bend and pouse2:54
Kisirani0:39
Boom party3:47
Nigina2:27
ONLY YOU JESUS5:44
Top stories
- Yopa freestyle
14 August
- Oxene Quiles feat kane gee
15 August
- Morning guys
16 August
- My new song is now out
14 August


Leave your comment