Mbosso Afichua Kitu Anachokikumbuka Zaidi Kutoka Kwa Costa Titch 


Mwandishi: Charles Maganga

Msanii kunako lebo ya WCB Mbosso Khan ametaja kitu anachokikumbuka zaidi kutoka kwa rapa Costa Titch wa Afrika Kusini ambaye aliaga dunia miezi michache nyuma. 

Rapa Costa Titch ambaye jina lake halisi ni Costa Tsobanoglou alifariki Machi 11 mwaka huu 2023 akiwa jukwaani huko Afrika Kusini baada ya kuanguka akiwa anatumbuiza na kushindwa kuamka tena. 

Costa Titch na Mbosso walikuwa ni marafiki wazuri na wawili hao walishirikiana kwenye ngoma mbili ambazo ni Moyo pamoja na Shetani ambayo inapatikana kwenye EP ya Mbosso ya kuitwa Khan. 

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano na Wasafi FM, Mbosso alidokeza kuwa moja ya vitu ambavyo anavikumbuka kutoka kwa Costa Titch ni hari yake kufanya kazi pamoja na uchangamfu aliokuwa nao muda wote. 

“Costa very smart, mcheshi, talented anapotaka kutoa kitu ana-deliver 100%. Vibe ukiwa nae studio lakini yeye alikuwa na vive stufio muda wote yani. Hajawahi kunionesha attitude ya aina yoyote. Tulikuwa karibu sana” alizungumza Mbosso 

Leave your comment