Biography Ya Beda Andrew, Safari Yake Ya Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Tuzo
12 May 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi-Charles Maganga
Jina Halisi : Beda Andrew
Jina La Kisanii : Beda Andrew Fabian
Alipozaliwa : Dar Es Salaam, Tanzania
Aina Ya Muziki : Gospel
Mwaka Alioanza Muziki : 2016
Maisha Ya Awali Ya Beda Andrew Yalikuwaje?
Beda Andrew ni msanii wa muziki wa Injili ambaye amezaliwa jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania na huku akiwa amekulia maeneo ya Kigamboni.
Kutokana na kuzaliwa kwenye familia ya kikristo Beda alianza kuimba akiwa mdogo sana ambapo alikuwa akiimba kwenye kwaya ya watoto hapo kanisani kwao maarufu kama Sunday School.
Lini Alianza Kazi Zake Za Muziki?
Akiwa anasoma kwenye shule ya Azania Secondary Beda alikuwa mchoraji mzuri sana lakini kadri muda ulivyokuwa unaenda pia kipaji chake cha kuimba kilizidi kuonekana.
Mara yake ya kwanza kuingia studio kurekodi wimbo ilikuwa ni mwaka 2013 kuelekea 2014 ambapo kupitia baba wa rafiki yake ambaye alikuwa ni Mchungaji, Beda aliweza kurekodi wimbo wake wa kwanza kwenye studio za Habari Maalum.
Mambo yaliendelea kuwa sukari kwa upande wake ambapo katika kutafuta nafasi zaidi pia alishiriki kwenye mashindano ya Gospel Star Search 2016
Kushinda Tuzo
Baada ya kutoa nyimbo tofauti tofauti mwaka 2016 Beda Andrew aliandika historia mpya kwenye muziki wa Injili nchini Tanzania baada y kushinda tuzo za Maranatha Awards huko nchini Kenya
Beda Andrew alikuwa ni miongoni mwa watanzania wa kwanza kabisa kushinda tuzo hizo. Kufikia sasa wasanii wengine kutoka Tanzania ambao walishawahi kuwania tuzo hizo (nomination) ni pamoja na Christina Shusho pamoja na Paul Clement.
Wasanii Waliomshawishi
Kwa mujibu wa Beda Andrew alidokeza kwamba kipindi anakua alikuwa anamsikiliza sana Rose Muhando na Jackson Benty.
Aidha katika moja ya mahojiano yake, Beda alidokeza kwamba anavutiwa sana mwimbaji kutokea nchini Marekani, Kirk Franklin hasa kwa namna ambavyo anaweza kutumbuiza live jukwaani.
Nyimbo Bora Za Beda Andrew Ni Zipi?
Daima Milele
Natamani
Nguvu Za Mungu
Nyumbani Mwako
Nayaweza
Nyumbani Mwako
Leave your comment