Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Rick Ross Adokeza Kufanya Remix Na Navy Kenzo
8 May 2023

[Picha: Instagram]
Mwandishi-Charles Maganga
DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3
Tasnia ya muziki nchini Tanzania imeendelea kunawiri na hii ni baada ya hivi karibuni msanii kutokea huko nchini Marekani, Rick Ross kuomba collabo kwa kundi la muziki Tanzania, Navy Kenzo.
Rick Ross ameomba collabo hiyo kutoka kwa Navy Kenzo hivi karibuni kwenye mtandao wa Instagram pindi Navy Kenzo na Rick Ross walipokuwa Insta Live.
Rick Ross ambaye jina lake halisi ni William Leonard Roberts III akiwa anazungumza na Navy Kenzo hivi karibuni amesema kuwa yuko tayari na angependa kushiriki kwenye remix ya “Sip N Whine” ambao ni wimbo namba 6 kwenye album ya Navy Kenzo ya kuitwa “Most People Want This “
Akiongea kwenye mahojiano na Fredrick Bundala, Nahreel alidokeza kuwa hakutegemea Rick Ross angependa ngoma hiyo na kuongeza kuwa anaamini remix ya wimbo huo wa “Sip N Whine” itakuwa kubwa zaidi.
Kufikia sasa mtanzania pekee ambaye amefanya ngoma na Rick Ross ni Diamond Platnumz kupitia “Wakawaka” ngoma ambayo iliteka hisia za wengi pindi ilipotoka.
Weekly Top 10 songs

Tudo Trocado3:17
CHAMPION GAL3:00
ONLY YOU JESUS5:44
Akaana kokukyalo2:21
Joy Is Coming3:08
Nasema3:02
BESTIE2:26
Minha Historia3:41
Baraka4:33
Nigina2:27
Top stories
- MCHUNGAJI
07 July
- News Flash
09 July


Leave your comment