Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

Wiki hii kwenye kiwanda cha Bongo Fleva bidhaa mpya zimeendelea kuchakatwa na bila shaka wasanii wamefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha mashabiki wanapata ladha tofauti tofauti za muziki. 

Kutoka kwa wasanii kama Country Wizzy, Roma Mkatoliki, Lody Music na wengineo wengi : 

Oright - Country Wizzy Ft Emtee 

Wiki hii Country Wizzy aliipeperusha vyema bendera ya Hiphop Tanzania baada ya kuunganisha nguvu na Emtee wa Afrika Kusini. Ngoma hii inatarajiwa kukita zaidi kwenye kumbi na sehemu mbalimbali za starehe Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla 
https://youtu.be/4q8relbx474

Roma Mkatoliki - Nipeni Maua Yangu 

Nipeni Maua Yangu ni ujio mpya wa Roma kwenye Bongo Fleva baada ya takriban miaka miwili ya ukimya wake. Humu ndani Roma anatupa mawe mazito kwa serikali akiwa anakosoa na kuonesha wapi kunahitaji marekebisho. 
https://youtu.be/S7zSplS-4j4

Phina - Rafiki 

Phina sio mzuri kwenye kuimba mapenzi pekee na kupitia wimbo wake mpya wa kuitwa “Rafiki” ameweza kuthibitisha hilo. Kutumia sauti yake mujarab Phina amezungumzia kuhusu marafiki wa kweli na utofauti wake na wasengenyaji. 
https://youtu.be/RPGbLhMOLeM

Simama - Lody Music

Kupitia “Simama” Lody Music anaelezea maumivu anayopitia baada ya kuachwa na mpenzi wake 
https://youtu.be/1eJ33bX19FE

Shobo - Lola Mziwanda 

Uzuri wa Lola Mziwanda ni kwamba ana uwezo wa kuimba kitu chochote na kwenye ngoma yake hii mpya, fundi huyu amezingumzia kuhusu watu ambao wanapenda sana kufuatilia maisha ya wenzao
https://youtu.be/fACNwG1cI-0

Leave your comment