Harmonize Adokeza Kuandaa Video 5 Zanzibar

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Harmonize amedokeza kwamba kwa sasa yupo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuandaa video 5 za muziki.

Taarifa hii kutoka kwa Harmonize inakuja siku chache tangu msanii huyo aachie video yake ya “Single Again” ambayo imezua mjadala mkubwa mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram upande wa Instastory, Harmonize alidokeza kwamba kwa sasa yuko visiwani Zanzibar kwa siku 10 na kwamba katika muda huo atashirikiana na Director Kenny kuandaa video za muziki takriban 5.

“Zanzibar Kuna Wamakonde Wengi Kuliko Kabila Lolote Litokalo Bara!!! MASAI ndio pengine wanatukaribia!!!!! Lol I'm Home!!!!!

Have 2B proud For Zanzibar a 10 Day's 100 5  VIDEOS @director_kenny Let's Go” aliandika Harmonize.

Ikumbukwe kuwa video ya Harmonize ya kuitwa “All Night” pia ilifanyika huko visiwani Zanzibar

Leave your comment