Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama unapenda muziki kutokea nchini Tanzania basi vaa tabasamu la aina yake kwani kwa wiki hii wasanii mbalimbali kutokea nchini humo kuanzia kwenye Bongo Fleva, Singeli na mitindo mingine ya muziki wameachia ngoma kali kwa ajili yako.

Kutoka kwa wasanii kama Meja Kunta, Mbosso, Lony Bway na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma mpya kutoka kwa wasanii wa Tanzania kwa wiki hii:

Khan Acoustic EP - Mbosso

Mbosso alinogesha wiki hiu kwa kuachia Khan Acoustic EP ambayo ni toleo jipya la EP ya Khan ya mwaka 2022. Khan Acoustic imesheni ngoma 3 ambazo ni “Huyu Hapa”, “Yule” na Wayo na katika ngoma hizi tatu Mbosso amejikita zaidi katika kuonesha ufundi wake wa kuimba kuliko kitu chochote.

https://www.youtube.com/watch?v=dbVw-9ZMOTs

 

Ushali - Meja Kunta, Kiduchu Mc & Elisha

Ushali ni muendelezo wa ngoma ya “Demu Wangu” ya kwake Meja Kunta ambapo humu ndani Kiduchu Mc anatumia maneno ya kuudhi na kauli zenye utata kujibu hoja za Meja Kunta kwenye ngoma ile ya “Demu Wangu”.

https://www.youtube.com/watch?v=dl1JPQwDmnI

Nakukumbuka - Lony Bway

“Nakukumbuka” ni moja ya kati ya ngoma za Bongo Fleva ambazo zimesukwa vyema na mashahiri yenye kugusa moyo. Humu ndani Lony Bway analalamika baada ya kuachwa na mwenza wake aliyekuwa anampenda sana

https://www.youtube.com/watch?v=1yCzez5t5TI

Ushindi EP - Goodluck Gozbert

Baada ya kuidokeza kwa muda kidogo hatimaye Goodluck Gozbert ameachia EP yake ya Ushindi ambayo imezua gumzo na kupokelewa vyema na mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania. Ushindi EP imesheheni nyimbo 8 ambazo ni “Kinamuuma”, “Kimya Kimya”, “Sikupanga” na nyinginezo nyingi.

https://www.youtube.com/watch?v=rag27LQpBkY

Na Iwe Kheri - Jay Melody

Jay Melody amerudi “Na Iwe Kheri” ngoma kali ambayo ndani yake Melody anasherehekea na kuwatakia waislamu wote mtu go mermaid wa mwezi Ramadhan

https://www.youtube.com/watch?v=-m46Xu6esJw

Leave your comment