Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Diamond Platnumz Adokeza Kuachia Ngoma Mpya Na Mabantu
5 April 2023

[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz hivi karibuni amedokeza kuachia ngoma mpya na kundi linalofanya vizuri Tanzania kwa sasa, Mabantu.
Hivi karibuni Mabantu waliachia EP yao ya kuitwa “University EP” ambayo ina ngoma 8 huku ngoma yao ya kuitwa “Shemeji” waliyomshirikisha Baddest 47 ikiwa inafanya vizuri zaidi. Mabantu limeundwa na wasanii wawili ambao ni Twaah na Muuh
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mabantu, wasanii hao walichapisha video inayomuonesha Diamond Platnumz akiwa na Mabantu ambapo Platnumz alisifia EP mpya ya Mabantu ya kuitwa University EP na kuongeza kuwa Mabantu ni wasanii wenye vipaji kikubwa na tayari amefanya nao ngoma.
“Mabantu ni miongoni mwa vijana wenye talent sana nchini na tuna nyimbo mimi na wao na nimewashirikisha na nafikiri you can tell me kuwashirikisha wao inamaanisha hawa watu wabaya sana ni miongoni mwa ngoma ambazo zitatoka mwaka huu yaani Ramadhan ikishaisha yaani hapa hakalikki” alizungumza Diamond Platnumz.
Kando na Mabantu, collabo nyingine ambazo zinasubiriwa kutoka kwa Diamond Platnumz kwa mwaka huu ni pamoja na ngoma ambayo ameshirikiana na Marioo, Baba Levo pamoja na G Nako.
Weekly Top 10 songs

Trust No One3:13
chile-one-so-lucky4:02
Kamwambie3:47
Joy Is Coming3:08
Buwooma2:44
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Leo3:39
Maringo4:00
NANI ft. Kamanda Pedeshee3:56
Top stories
- The Marathon
25 April
- Who Is Bad Beric
24 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April
- MOSS Kay
24 April


Leave your comment