Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Victoria Kimani Adokeza Collabo Mpya Na Wasanii Wa Tanzania
4 April 2023

[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Msanii wa muziki kutokea nchini Kenya Victoria Kimani hivi karibuni amedokeza kwamba Tayari ameshafanya collabo na wasanii wawili kutokea hapa nchini Tanzania.
Victoria Kimani ambaye mwaka 2021 alitetemesha Africa kupitia albamu yake ya “Spirit Animal” amedokeza kwamba kuna collabo inakuja kati yake na wasanii wawili wakubwa kutoka Tanzania. Victoria Kimani kwa sasa yuko nchini Tanzania kwa ajili ya mapumziko.
Akizungumza hivi karibuni kwenye kipindi cha The Switch, Victoria Kimani amedokeza kuwa ameshafanya collabo na wasanii wawili kutoka Bongo ambao hakuwataja na kuongeza kuwa kuna baada ya wasanii aliwaomba collabo lakini walikataa
“Kwa sasa nimeshafanya collabo na wasanii kutoka Tanzania. Nilishawahi kufanya hivyo pia zamani. Kuna baadhi niliwatafuta kwa ajili ya collabo lakini nadhani walijiona ni wakubwa sana. SiweI kuwataja” alidokeza Victoria Kimani
Ikumbukwe kuwa mwaka 2014 Victoria Kimani aliachia ngoma ya “Prokoto” ambayo aliwashirikisha Diamond Platnumz pamoja na Ommy Dimpoz.
Weekly Top 10 songs

Inama4:58
ONLY YOU JESUS5:44
Bikyaganye3:29
Mshamba2:44
Daddy2:50
Sissa3:37
Eazzy Ft Way Dee2:59
Alaska2:29
Come Alive3:32
Deep House BLACK5:35
Top stories
- KACHUMBALI ARMY(Kiswahili)
08 October
- KACHUMBALI ARMY
08 October
- My incoming songs
09 October
- USINIACHE
09 October



Leave your comment