Zuchu Ni Fundi : Haya Ndio Mafanikio Ya Zuchu Tangu Aanze Muziki

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kwa sasa Zuchu, ameishika Bongo Fleva mikononi mwake. Ngoma zake nyingi hupenya haswa kwenye masikio ya mashabiki na kwenye mitaa na kumbi mbalimbali za starehe Tanzania ni jambo la kawaida sana kusikia ngoma kama Kwikwi, Fire, Utaniua na hata Cheche zikirindima.

Malkia huyu kutoka WCB alitambulishwa rasmi kwenye lebo hiyo Aprili mwaka 2020 na tangu hapo hajawahi kurudi nyuma.

Pamoja na ukweli kwamba umaarufu wa Zuchu umechagizwa na ushawishi alionao Diamond Platnumz pamoja na mipango kabambe ya Mameneja wake kama Sallam SK na Doris Mziray lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba Zuchu ana kipaji kikubwa mno.

Katika mwezi huu ambao Mdundo inasherehekea na kutambua mchango wa wanawake katika muziki, haya ni baadhi ya mafanikio ya Zuchu tangu aanze muziki :

Tuzo

Zuchu ni mshindi wa tuzo tofauti tofauti ikiwemo AFRIMMA ambapo kwa mwaka 2020 alishinda kama msanii bora chipukizi kwenye tuzo hizo huku mwaka 2022 alishinda kama msanii bora wa kike katika tuzo hizo hizo za AFRIMMA

Youtube

Zuchu ndio msanii wa kike anayeongoza kwa kuwa na subscribers/wafuatiliaji wengi zaidi Afrika kwenye mtandao wa Youtube na kufikia sasa ndiye msanii wa kike Tanzania na Afrika Mashariki anayeongoza kutazamwa zaidi kwenye mtandao huo.

Aidha kwa mwaka 2021, video yake ya Sukari ilikuea ndio video ya muziki iliyotazamwa zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara

Ubalozi

Tangu aanze muziki, Zuchu amelamba ubalozi wa kampuni kubwa na bidhaa mbalimbali.

Baadhi ya kampuni hizo ni pamoja na Darling Hair, kampuni ya simu ya Infinix pamoja na Wasafi Bet.

Mitandao Ya Kijamii

Zuchu ni moja ya wasanii wa kike wenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram ambapo ana wafuasi zaidi ya Milioni 5.4 na wafuasi hao amewakusanya chini ya miaka mitatu.

Ngoma za Zuchu pia hutamba na kutumika zaidi kwenye mtandao wa Tik Tok huku ngoma yake ya Kwikwi ikiwa imetumika kwenye video ya laki mbili tu.

Matamasha

Zuchu ni moja ya wasanii wa kike Tanzania ambao wameshatumbuiza kwenye majukwaa makubwa Tanzania.

Novemba 2021, Zuchu alitumbuiza kwenye tuzo za AFRIMMA.  Mwaka 2022 alitumbuiza kwenye jukwaa la Africa Day Concert ambalo huandaliwa na Youtube huku mwanzoni mwa mwaka 2023 alitumbuiza kwenye tuzo za Soundcity za huko nchini Nigeria

Collaboration

Kufikia sasa Zuchu ameshashirikiana na wasanii wa ndani ya Tanzania ikiwemo Diamond Platnumz, Mbosso na Khadija Kopa.

Upande wa kimataifa, Zuchu ameshashirikiana na wasanii tofauti tofauti ikiwemo Joe Boy, Olakira, Adekunle Gold na wengineo wengi.

Leave your comment