Borussia Dortmund watangaza vita kumbakiza Bellingham Dortmund -Mdundo Alt

[Picha: Goal.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mkurugenzi wa klabu ya Borussia Dortmund Sebastian Kehl ameuthibitishia umma kwa kuweka waza juu ya taarifa za klabu hiyo kutaka kuongeza mkataba na kiungo Jude Bellingham katika viunga vya Signal Iduna Park.

Taarifa hiyo aliiweka hadharani wakati wa mahojiano dhidi ya kituo cha habari Cha ZDF kutokea Ujerumani na kusema kwa sasa mchezaji huyo mwenye uraia wa Uingereza amejikita katika mpira na uongozi wa timu hiyo wakijipanga kwa ajili ya mahojiano ya kuongeza mkataba wake yatakayofanywa huku familia yake ikihusishwa.

Mwaka 2020 Jude alijiunga na Borussia Dortmund akitokea Birmingham ya Uingereza na akiwa Dortmund amekuwa mmoja wa wachezaji wenye umri mdogo pamoja na uwezo mkubwa akiwa uwanja huku nidhamu yake ikipelekea Kupewa kitambaa Cha unahodha.  Pia kutokana na kiwango hicho kimemfanya kucheza kombe la Dunia mwaka 2022 akiwa na timu ya Taifa ya Uingereza na dau la Jude limezidi kwenda hewani tangu mashindano hayo ya kombe la Dunia kukamilika.

 

Mbali na Borussia Dortmund kutaka kumkalisha Jude Signal Iduna lakini pia Kuna vilabu vingine haswa vya Uingereza vikisemekana kupendezwa na mchezaji huyo hivyo mate yanawatoka wakimtaka nyota huyo katika vilabu vyao. Baadhi ya vilabu hivyo ni pamoja na Majogoo wa London Liverpool, Newcastle pamoja na Los Blancos Real Madrid ya Uhispania.

Leave your comment