Ubashiri Mechi ya Manchester United Vs Westham United -Mdundo Alt

[Picha: Khelnow.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mbio zingine Tena zinaendelea katika kombe la FA wakati Manchester United watakapo vaana na Westham United ukiwa ni mzunguko wa tano wa kinyang'anyiro cha kombe hilo.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza Baada ya Mashetani hao wekundu kushinda kombe la Carabao siku ya Jumapili dhidi Newcastle na ushindi huo wakiutaja kama ni mbio za vikombe vingine ikiwemo Kombe la FA.

West ham Kwa upande wao wanajitahidi kujikongoja katika ligi wakipoteza mchezo mmoja, wakitoa sare michezo miwili na kushinda mechi mbili katika michezo mitano ya hapo kabla. Kwa upande wa kutoshana nguvu United na Westham, Mashetani wekundu wameshinda michezo minne na West Ham kushinda mchezo mmoja katika michezo mitano ya hapo awali.

Katika kikosi Cha David Mayos wachezaji wake wawili Maxwell Cornet pamoja na Kurt Zouma ndio wenye uwezekano wa kutokuwepo katika kikosi cha mechi hiyo kutokana na majeruhi.

United wao Anthony Martial amerejea mazoezini akitokea Kuwa majeruhi huku wachezaji wale wale wa Manchester ambao ni Christian Eriksen pamoja na Don Van de Beek wakiendelea kukosa mechi mbalimbali.

Katika mchezo huu United kutoa sare au kushinda mchezo odds ni 1.17

Leave your comment