Ubashiri Mechi ya RB Leipzig Vs Manchester City -Mdundo Alt

[Picha: Skysports]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Utamu wa ligi ya mabingwa Ulaya unaendelea kunoga na Jumatano Hii Manchester City wanakwea pipa hadi Ujerumani kama wenyeji wa Red bull Leipzig katika uwanja wa Red bull Arena.

Wakiwa nafasi ya tano Leipzig tangu walipopoteza mechi Yao ya mwezi Septemba dhidi ya Borussia M'gladbach tayari wameshinda michezo 18 na kutoa sare michezo minne kabla ya Union Berlin kuwapa kichapo Cha bao mbili kwa Moja.

Kwa upande wao The Citizen tayari wakiwa wanalinyemelea kombe la ligi kuu Uingereza Bado moto wao Si wa kubezwa licha ya sare Yao dhidi ya Nottingham Forest kuwashusha mpaka nafasi ya pili katika ligi hiyo.

Timu Hizo mbili tayari wameshacheza michezo miwili na yote ikiwa michezo ya ligi ya mabingwa Ulaya na City alifanikiwa kufunga mechi ya kwanza lakini pia Rb Leipzig wakalipiza kisasi katika mchezo uliofuata kwa ushindi wa bao 2 kwa Moja.

Wakiwa nyumbani majeruhi wa Mjerumani Marco Rose ni pamoja na mlinda mlango Peter Gulacsi, beki Abdou Diallo, pamoja na kiungo kutokea Hispania Dani Olmo.

Utamwambia Nini bwana mkubwa Guardiola akiwa na majeruhi mmoja pekee John Stone huku nyota wake wakubwa uwanjani kama Haaland na mmwaga maji wake Kelvin de Bruyne wakiwa imara?

Odds za Manchester City kushinda mchezo huu ni 1.80.

 

Leave your comment