Thierry Henry Atoa Ushauri Mzito Kwa Haaland - Mdundo Alt

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya ushindi wa Manchester City dhidi ya Arsenal, sasa timu hiyo imepaa Moja kwa Moja Hadi kileleni na kushika usukani wa Ligi kuu ya Uingereza.

City ambao pia ni mabingwa watetezi wa ligi kuu hiyo wameweza kuwapiku Arsenal baada ya ushindi wa mabao matatu kwa Moja mchezo uliopigwa katika viwanja wa Emirates stadium. Katika mchezo huo Arsenal waliopata bao lao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penalti uliowekwa kambani na Bukayo Saka.

Sasa basi wakati wa uchambuzi wa mechi mbalimbali uliowahusisha wachambuzi ngulu wa soka kutokea CBS  Sports Golazos ambao ni Thierry Henry, Jamie Carragher, Micah Richards wakiongozwa na mwanadada Kate Abdo waliweza kugusia suala la Erling Halaand na upatikanaji wa mabao yake katika mechi za City.

Henry ambaye pia alichezea timu ya Arsenal hapo miaka ya nyuma alimtaka Halland kutafuta njia zaidi za ufungaji kuliko kutegemea pasi za usaidizi wa magoli ambazo mara nyingi zinatoka kwa Kelvin De Bruyne. Pia alitolea mfano wakati akiwa chini ya kocha Arsene Wenger ambaye akimuuliza endapo timu yake itashindwa kumtengenezea njia mzuri za ufungaji ni Nini atafanya?

Katika kulijibu swali hilo Henry alimshauri straika huyo ambaye pia ni kinara wa mabao Uingereza kwa kuanza kumsifia Halaand na kusema "……Unaweka mpira ndani ya boksi unamlisha unakufa,...angani, ardhini……Manchester City kwa sasa wanatabirika ila sijasema unaweza kuwasimamisha kwa urahisi….'. Thierry Henry aliueleze uwezo wa Erling Halaand lakini pia akionesha ni kwa jinsi gani timu hiyo imekuwa ikitabirika kurahisi wakati wa mashambulizi.

Pia Henry aliongeza kwa kuelezea umuhimu wa mchezaji mmoja mmoja katika mchezo wanapokuwa uwanjani na kuacha kutegemea mtu mmoja katika upatikanaji wa matokeo. Hivyo aliongeza kwa kusema  …siyo muda wote ni kuhusu magoli, ni kuhusi ni Nini utaleta kwenye timu..."

Mbali na hayo yote kwa sasa 'Golden boot' inauelekea upepo wa mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 akiongoza kwa kuwa na jumla ya mabao 25 huko  EPL.

Leave your comment