Mabosi Wa Qatar Kumiliki Manchester United- Mdundo Alt

[Picha: Twitter]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Huenda maombi ya mashabiki wengi wa Timu ya Manchester United yakatimilika baada ya mwanahabari kutoka Qatar kuchapisha picha ya klabu hiyo katika ukurasa wake wa Twitter na kuacha ujumbe wenye utata juu ya ukamilishwa wa mpango wa kuuzwa kwa Klabu hiyo ya mashetani wekundu.

Kabla ya mechi ya Barcelona na Manchester United kumalizika kwa sare ya bao mbili, mwanahabari na mhariri kutokea Doha, Qatar Majed Al Khelaifi alichapisha picha ya nembo halisi ya Manchester United na kuacha ujumbe uliosema "Man United, Qatari". Ujumbe huo unaweza kuinua upya tumaini kwa Mashabiki wa United ambao wamekuwa wakipinga vikali timu hiyo kuendelea kuwa chini ya 'Glazer Family'

Sambamba na Hilo pia wiki chache zilizopita familia hiyo ilitoa tangazo la kutaka kuiuza timu hiyo huku kiasi cha Euro bilioni 5 zikitakiwa kuwekwa kibindoni ili kukamilisha ununuzi huo. Pia Glazer waliongeza ya kuwa fedha hizo zitatumika pia katika shughuli nzima za maboresho ya Uwanja wa Old Trafford kama siyo ujenzi kamili.

Kwa kumbukizi za hapo awali kidogo Glazer wamekuwa wakichukiwa na mashabiki kindakindaki wa timu hiyo ambao wanaituhumu familia hiyo kuiingiza timu hiyo katika madeni.

Aidha dili hilo linatarajiwa kuendelea na mchakato wake siku ya Ijumaa huku wawekezaji hao wakitarajiwa pia kukamilisha mchakato mzima wa umiliki wa klabu hiyo kabla ya mwezi huu wa wapendanao kumalizika.

Leave your comment